/*Start Css Menu*/ .menu{ border:none; border:0px; margin:0px; padding:0px; font-family:verdana,geneva,arial,helvetica,sans-serif; font-size:14px; font-weight:bold; color:8e8e8e; } .menu ul{ background:url(http://3.bp.blogspot.com/-jEZvPu90bIA/TjlATeBIGoI/AAAAAAAAE4A/shxxdvs2fHI/s1600/menu-bg.gif) top left repeat-x; height:43px; list-style:none; margin:0; padding:0; } .menu li{ float:left; padding:0px 8px 0px 8px; } .menu li a{ color:#666666; display:block; font-weight:bold; line-height:43px; padding:0px 25px; text-align:center; text-decoration:none; } .menu li a:hover{ color:#000000; text-decoration:none; } .menu li ul{ background:#e0e0e0; border-left:2px solid #a80329; border-right:2px solid #a80329; border-bottom:2px solid #a80329; display:none; height:auto; filter:alpha(opacity=95); opacity:0.95; position:absolute; width:225px; z-index:200; /*top:1em; /*left:0;*/ } .menu li:hover ul{ display:block; } .menu li li { display:block; float:none; padding:0px; width:225px; } .menu li ul a{ display:block; font-size:12px; font-style:normal; padding:0px 10px 0px 15px; text-align:left; } .menu li ul a:hover{ background:#949494; color:#000000; opacity:1.0; filter:alpha(opacity=100); } .menu p{ clear:left; } .menu #current{ background:url(http://1.bp.blogspot.com/-NjNjSmAlq34/TjlATMvGF7I/AAAAAAAAE38/UxPs9Qg4Fyg/s1600/current-bg.gif) top left repeat-x; color:#ffffff; } /*End Css Menu from http://www.spiceupyourblog.com*/

Powered by Blogger.

Mahaba


SIFA MUHIMU ZA KUZINGATIA UNAPOTAFUTA MTU WA KUISHI NAYE!!


         MARA nyingi vijana hupata taabu sana katika suala la kuchagua mchumba. Vijana wa kiume ndio hasa hupata wakati mgumu zaidi kwani jamii imewapa wajibu wa kuanzisha mazungumzo yahusianayo na mapenzi. Hata hivyo, vijana wa kike nao wanao wajibu wa kuchagua ili kuhakikisha kuwa hawaanguki mikononi mwa mabazazi wa kuwalaghai na kuwatumia kwa raha za miili yao kisha kuwaacha kwenye mataa.

Ni jambo la kawaida kwa vijana walio wengi, wawe wa kike au wa kiume, kuangalia sura na mwonekano wa mtu. Lakini unapotafuta mchum ba kwa malengo ya kuishi naye maisha yako yote kama mume na mke haipendezi kuangalia tu mwonekano, maana Waswahili husema si kila king’aacho ni almasi. Kwa sababu hiyo, hapa yatabainishwa mambo muhimu ya kuangalia na kuzingatia katika suala hili.

1. UADILIFU
Pamoja na sifa zote za uzuri zinazoweza kubainishwa na kufanywa kuwa vigezo vya uzuri wa mwanamke na mwanaume na hata zikatumiwa kumpata Miss au Mr Tanzania, sifa kuu impasayo mtu anayefaa kuwa mchumba kuwa nayo ni sifa ya uadilifu.
Mtu anapokuwa na uadilifu (pengine uaminifu), maana yake ni kwamba tabia ya mtu huyu anayoionesha nje ndiyo tabia yake halisi na anapofanya jambo jema analifanya kwa roho yake na si kwa unafiki.
Mtu anapokuwa mwadilifu ataheshimu maadili na kufanya wema, hata pale inapokuwa rahisi kwa wengine kukengeuka na kufuata njia za mkato ambazo mara nyingi si za halali.
Mtu mwadilifu pia huwa na sifa za ukweli na kujitolea kuwasaidia watu wengine bila kujali faida – haya yote ni mambo muhimu ambayo mtu mwenye kuwa nayo huwa na msingi wa ujenzi wa uhusiano imara na wa kudumu.
Watu wanaoweza kujivunia furaha ya kweli katika maisha yao ya ndoa, ni watu ambao wamekutana wote wakiwa na sifa ya uadilifu ambayo hujumuisha mambo mengi.
Zipo ndoa nyingi zenye furaha ya bandia. Furaha hii mara nyingi hutokana na ridhiko la kimwili alipatalo mtu kutokana na kukidhiwa kwa mahitaji yake ya kimwili yanayohusiana na haki za msingi za binadamu – yaani chakula, mavazi na malazi. Lakini furaha ya kweli ya maisha ya ndoa, watu hawaipati isipokuwa katika uhusiano ambao wenza wamethibitishana kuwa waadilifu.

2. HEKIMA
Mtu mwenye uadilifu wa kweli, mbali na kuwa mwema kwa mwenzake, pia huhakikisha anakabiliana kwa busara na hekima na matatizo yote yanayoweza kusababisha kuyumba kwa uhusiano, hususan yale yaliyo nje ya uwezo wake.

Uzoefu unaonesha kuwa wapenzi, hususan wanandoa walio katika uhusiano wa muda mrefu wanaoendelea kufurahia unyumba wao si wale ambao walipendana kwa mvuto na wala hawana mambo mengi ya asili yanayowaunganisha kuliko wale wanaotengana. Lakini la muhimu ni kwamba watu hawa huwa wamejifunza jinsi ya kukabiliana kwa hekima na matatizo yanayojitokeza, hususan yale yanayotokana na tofauti zao kimtazamo.

Ukiachilia mbali sifa ya uadilifu, watu hawa huwa wamejifunza kukabiliana na matatizo kuhusiana na uzazi na ulezi wa watoto, uhusiano na ndugu, jamaa na marafiki, suala la ngono, fedha na maisha ya unyumba kwa ujumla.

Habari njema ni kwamba uadilifu na hekima ni mambo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza na kisha kufanyia kazi. Ndiyo maana wanandoa hufundishwa kabla ya ndoa na hata wanapokuwa tayari wameoana huendelea kuhudhuria semina za kidini na kijamii kwa ajili ya kujiimarisha.

Kwa hiyo, kama mume/mke wako mtarajiwa anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kuhusiana na jinsi ya kuishi na mtu wa jinsia nyingine, ana nafasi kubwa ya kuwa mke/mume mzuri baadaye.

3. UPOLE
Mfalme Suleiman katika mojawapo ya semi zake za hekima alisema mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake. Yamkini ndivyo ilivyo pia kwa mwanaume mpumbavu, maana upumbavu haujengi.
Siku zote kitu kinachovunja uhusiano wa kindoa si makombora ya nyuklia, bali ni ulimi. Kwa kadri mtu anavyoutumia ulimi wake anaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yake.
Katika kumwangalia mtu ambaye unaweza kujenga naye nyumba ya kudumu, ni vema kumchunguza na kuhakikisha kuwa si mtu mwenye kupenda kurefusha maneno, maana hakika huyu atasababisha ugomvi mara kwa mara na uhusiano hautadumu.

Wapo watu ambao ndoa zao zina sifa ya ugomvi na karibu kila mtu anafahamu na hata wamekuwa kero kwa ndugu, jamaa na majirani zao, mara kwa mara wakiwaamsha watu usiku wa manane wakitafuta suluhu.

Mara nyingi wanaume ndio huanzisha ugomvi, lakini ugomvi huwa na nguvu zaidi kama mwanamke ni msemaji. Dawa ya kuzuia ugomvi usiokuwa na mpango ni kupunguza maneno na kuepuka kutafuta ushindi katika ubishi. Lakini kinga ya tatizo hili ni kuepuka kujiingiza katika uhusiano na mtu ambaye umejihakikishia kuwa si mwingi wa maneno.

Bahati nzuri, jamii huwatambua wanawake/wanaume ambao wanaweza kuwa wake/waume bora baadaye kwa hiyo ni wajibu wa mtafutaji kuhakikisha kuwa anafanya uchunguzi wa kina kabla ya kujitosa kwa mtu ambaye baadaye atamtaabisha.

Mwanandoa aliyeifahamu vema dhana ya ndoa – kwamba ni maisha ya kuvumiliana na kuchukuliana, hufahamu ni wakati gani wa kusema na wakati gani wa kukaa kimya. Mtu huyu pia hufahamu njia nzuri na salama ya kujiondoa kwenye tatizo anapoona mwenzake anaelekea kubaya, ili hatimaye uhusiano wao uendelee kuwa salama japo wao wanaweza kuwa wamekwaruzana.

Mtu huyu mwenye upole hujiweka katika mkao wa upatanishi na huhakikisha kuwa kila mjadala mkali unapita na kumalizika salama. Ni wazi kuwa katika kutafuta, kama hukukurupuka, utamwona mtu mwenye hulka hii – upole.

4. MVUTO

Hisia za mvuto wa kimapenzi ni muhimu katika kujenga uhusiano. Mtu mmoja akauliza, ni yupi bora – yule anayenivutia sana au yule anayenipenda sana? Maisha ni ya ajabu sana. Huwa inatokea kuwa mtu unayevutiwa naye sana yeye havutiwi nawe, bali anavutiwa na mwingine ambaye naye hana mpango naye!

Haya ndiyo maisha. Uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya watu walio katika ndoa hawajawaoa/kuolewa na watu waliokuwa wakiwapenda sana enzi za ujana wao, au wale waliotimiza ndoto za ujana wao. Bahati njema miongoni mwa wanandoa hawa wapo wale wenye ndoa imara sana.

Mvuto wa kimapenzi ni muhimu sana, lakini watu husema maji yakisema usininywe yajibu kuwa wewe pia huna kiu nayo. Japo inaweza kuonekana kama ni aina ya ‘sizitaki mbichi hizi’ lakini si vema kujisumbua na mtu asiyekupenda.

Badala ya kujihangaisha na mtu asiyekupenda, kaa chini na umsubiri anayekupenda hata kama huhisi kuvutiwa naye sana. Baadaye utamzoea na maisha yatakuwa mazuri, kisha utajiuliza baadaye yule aliyekuringia alikuwa na nini cha ziada?

Lakini iwapo mambo mengine yote yatakwenda sawa, ni vema na muhimu kabisa kuhakikisha kuwa mtu unayepanga kuwa naye maisha yako yote ni mtu anayekuvutia kimwili na kiakili, maana vinginevyo unaweza kupata sababu ya kukidhi kiu yako nje – jambo ambalo si maadili mema katika ndoa na maisha.

NI MUHIMU KUWA MAKINI

Katika nyakati za ujana, watu wengi hubabaishwa kwa mengi. Vijana wa kiume hubabaishwa na sura, maumbile na pengine rangi na kusahau mambo muhimu yaundayo orodha ya sifa za mke mwema.

Kwa upande wao, vijana wa kile pia waweza kubabaishwa na pesa, maumbile, sura, utanashati, umaarufu au kuchoshwa na shinikizo la umri, hivyo kujikuta wakijitumbukiza kwa wanaume wasio na sifa za waume wazuri.

Lakini tukirejea kwenye msemo wa zamani kuwa uzuri si hoja bora tabia, ni wazi kuwa tutafikia mahali tutajenga mahusiano imara na yasiyotikiswa na sunami zozote za kimaisha. Ilimradi tu uhakikishe kuwa mtu mwenyewe anakupa mvuto kimapenzi, maana vinginevyo kutakuwa hakuna maana.

MAISHA NDIO HAYA SIO MAIGIZO,TAFAKARI KWANZA!!!!!!!!!

1 comments: